Tangazo hilo lime tolewa baada ya Marekani, Ufaransa na Uingereza, kushambulia Syria kwa makombora, kwa sababu ya madai kuwa serikali ya Syra ilitumia silaha za kemikali katika shambulizi mjini Douma.
Naye rais wa urusi Vladimir Putin, ambaye ni mshiriki wa karibu wa rais Assad, ameonya kuwa mashambulizi ya ziada kutoka mataifa ya magharibi dhidi ya Syria, ita leta uharibifu katika maswala ya dunia.
Rais Putin pamoja na mshiriki wake wa Iran, Hassan Rouhani wamesema kuwa mashambulizi hayo, yame haribu fursa zakupata suluhu yaki siasa katika mgogo wa Syria amabo ume dumu kwa muda wa miaka misaba.