Nao wakenya wanao ishi nchini Australia, wame kuwa wakifuatilia kwa karibu, kampeni, upigaji kura na sasa hesabu za kura hizo.
Katika mazungumzo maalum kwenye jopo la uchaguzi mkuu wa Kenya, wawakilishi wa mirengo mikuu yakisiasa ya Kenya walifunguka kuhusu fursa za wagombea wao kuibuka washindi katika uchaguzi huo pamoja na matarajio ya uongozi wa vinara wa mirengo wanayo pendelea.
Kufikia wakati wakuchapisha makala haya, matokeo rasmi yalikuwa hayaja tangazwa na tume huru la uchaguzi wa Kenya IEBC. SBS Swahili itachapisha matokeo rasmi ya uchaguzi huo punde tutakapo yapokea.