Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Doroth Gwajima amesema : ““Wizara ya Afya haina mpango wa kupokea chanjo ya Covid 19 inayoripotiwa kuwepo na kutumika katika mataifa mengine, ifahamike kuwa Serikali kupitia Wizara ya Afya inayo taratibu za kufuata pale inapotaka kupokea bidhaa yoyote ya afya baada ya Serikali kujiridhisha hivyo kwa nia njema kabisa ni hadi tujiridhishe na si vinginevyo.”
Nako nchini Uganda, mwanasiasa Robert Kyagulanyi anayejulikana pia kwa jina lausanii Bobi Wine, amefikisha hoja mahakamani kuomba matokeo ya uchaguzi mkuu yafutwe, na uchaguzi mpya uandaliwe kwa sababu ya madai ya wizi wa kura.
Bofya hapo juu kwa taarifa kamili.