Vikundi hivyo vime dai kuwa sheria hizo zita fanya iwe vigumu kwa wahamiaji kuishi nchini Australia.
Kuanzia julai mwaka ujao, wahamiaji wapya wata subiri miaka mitatu kabla yaku weza kupokea malipo ya ustawi, hali ambayo ni nyongeza ya mwaka mmoja kwa muda wa sasa waku subiri kwa miaka mbili.





