Tangazo hilo lita fanywa mwezi mmoja mapema, kabla ya uchaguzi mkuu utakao fanywa mwezi Mei.
Kupata hisia kuhusu kile ambazo wapiga kura wakongwe wata tazamia katika bajeti hiyo, shirika la habari la SBS lilitembelea eneo bunge la Corangamite jimboni Victoria. Eneo bunge hilo liko chini ya uongozi wa mbunge wa chama cha Liberal, ambaye uwezo wake waku tetea wadhifa wake uko mashakani.
Sera ya chama cha Labor yakupiga marufuku mikopo ikishinda uchaguzi, imewaacha baadhi ya walio staafu katika eneo bunge hilo, kuanza kufikiria usalama wao kifedha.
Ukosefu wa uaminifu unaweza gharimu, pande zote zakisiasa ushindi katika uchaguzi mkuu.