Kiongozi wa chama cha Labor Anthony Albanese, alirejea katika harakati za kampeni baada ya wiki nzima yakujitenga baada yakupatwa na UVIKO-19. Wakati huo huo viongozi wawili wa vyama vikubwa nchini wame endelea kujadili lini watafanya mjadala mwingine wakitaifa. Mivutano katika ukanda wa Pasifiki nayo, ime endelea kuongezeka kuhusu jinsi Australia ilivyo simamia mkataba wa usalama.
Wiki ijayo itajumuisha mijadala kadhaa kuhusu sera kati yamawaziri na mawaziri kivuli, na kuna uwezekano kutakuwa mjadala mwingine kati ya Scott Morrison na Anthony Albanese. Ila mjadala kuhusu uwezekano wa mijadala, umezuia tarehe ya mjadala kuamuliwa. Waziri Mkuu amekubali kufanya mjadala kupitia vyombo vya habari kama Channels 7 na 9, ila Bw Albanese anapendekeza mjadala ufanywe katika kikao chakitaifa cha waandishi wa habari.
Bw Albanese alifanya vizuri zaidi katika mjadala wa kwanza wiki jana dhidi ya waziri mkuu hata hivyo, mjadala wa pili itabidi ufanywe haraka zaidi kabla ya siku ya uchaguzi mkuu itakayo kuwa katika wiki 3 zijazo.