Bw Yves, ni mmoja wa viongozi wa vijana kutoka jamii yawatu kutoka Afrika ya kati wanao ishi Australia. Katika mazungumzo maalum kwenye kongamano lakidini aliweka wazi umuhimu wa vijana kuendelea kushiriki katika maswala yakidini pamoja nakujumuika na wenzao.
Bw Yves alifunguka pia kuhusu umuhimu wa viongozi kuwa na mipango na mbinu mbadala, zakuwavutia vijana katika hali mbali mbali za maisha bila kutegemea dini tu kuwa kivutio.
Aliongozeza pia umuhimu wavijana kujumuika na wenzao, badala yakujitenga akisisitiza kuwa "mtu anaweza fika mbali akiwa mwenyewe, ila akiwa pamoja na wengine anaweza fika mbali zaidi."
Bonyeza hapo juu kwa mahojiano kamili.