Taarifa mpya kuhusu COVID-19: Queensland yarekodi ongezeko kubwa zaidi za kesi.

Hii ni taarifa mpya kuhusu Coronavirus nchini Australia kwa 1 Agosti 2021.

Dr Jeannette Young, afisa mkuu wa afya wa Queensland azungumza na waandishi wa habari mjini Brisbane, Jumapili, 1 Agosti, 2021

Dr Jeannette Young, afisa mkuu wa afya wa Queensland azungumza na waandishi wa habari mjini Brisbane, Jumapili, 1 Agosti, 2021 Source: AAP Image/Jason O'Brien

  • Mamlaka jimboni NSW wanafanya juhudi kuwa na na kiwango cha 80% ya chanjo.
  • Idadi kamili ya kesi za Delta jimboni Queensland ni 18.
  • Kesi nne mpya za Victoria zina ungwa na milipuko ya sasa.
  • Zaidi ya 40% yawa Australia ambao wana miaka 16 na zaidi, wamepokea chanjo yao ya kwanza.

New South Wales
NSW imerekodi kesi mpya 239 ndani ya jamii na angalu watu 61 walikuwa katika hali ambukizi ndani ya jamii kwa muda. Zaidi ya nusu ya kesi mpya chanzo cha maibukizi yazo haijulikani.

Dr Jeremy McAnulty kutoka idara ya afya ya NSW amesema, idadi ya watu 54 wanapokea huduma ya wagonjwa mahtuti na watu 49 walikuwa hawaja chanjwa. 

Kiongozi wa NSW Gladys Berejiklian amethibitisha kuwa serikali ya jimbo hilo, inaweza anza tekeleza malengo ya baraza lamawaziri kwa viwango vya chanjo vya kati ya 70%-80% miongoni mwa watu wazima katika umma.

Queensland
Queensland imerekodi kesi mpya tisa ndani ya jamii, ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya visa ndani ya jamii katika zaidi ya mwaka.  

Dr Jeanette Young ndiye afisa mkuu wa afya jimboni Queensland, amesema “kesi zinaongezeka kwa kasi", na amehamasisha wanachama wa jamii wajipimishe. 

Maeneo 11 ya halmashauri za jiji katika eneo la Kusini Mashariki Queensland, ziko chini ya makatazo ya siku tatu na, kwa sasa maeneo hayo yanazingatiwa kama sehem za hatari kitaifa, hali ambayo imefanya maeneo hayo yafuzu kwa misaada yakifedha.

Hali ilivyo kuwa nchini Australia katika masaa 24 yaliyo pita
  • Victoria imerekodi kesi mpya nne ndani ya jamii, kesi zote zikiwa zina ungwa na milipuko ya sasa, na zote zilikuwa ndani ya karantini wakati zilikuwa katika hali ambukizi.

  • Takwimu mpya zinaonesha kuwa zaidi ya 40% yawa Australia ambao wana zaidi ya miaka 16, kwa sasa wamepokea dozi yao ya kwanza ya COVID-19.


Karantini, safiri, zahanati za vipimo na, malipo ya janga

Karantini na masharti yavipimo yana simamiwa nakutekelezwa na serikali zamajimbo na mikoa:


ACT Safiri na Karantini
NT Safiri na Karantini
QLD Safiri na Karantini
SA Safiri na Karantini
TAS Safiri na Karantini
WA Safiri na Karantini
Kama unataka safiri ng'ambo, unaweza wasilisha ombi mtandaoni kupewa ruhusa. Bonyeza hapa kwa taarifa zaidi kuhusu masharti yakuondoka Australia. Kuna hatua za mpito kwa safari za ng'ambo, ambazo hutathminiwa mara kwa mara na serikali na, taarifa mpya huchapishwa kwenye tovuti ya Smart Traveller.





Tazama rasilmali zilizo tafsiriwa na huduma yamawasiliano ya Idara ya Afya ya tamaduni mbalimbali ya NSW 


Zahanati za vipimo katika kila jimbo na mkoa:


NSW 
ACT 

Pata hapa taarifa kuhusu malipo ya janga katika kila jimbo na mkaoa:

NSW 
ACT 

Share

Published

Updated

By SBS/ALC Content, Gode Migerano
Presented by Gode Migerano
Source: SBS

Share this with family and friends


Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service