Rural landscape, Western Australia, Australia
Rural landscape, Western Australia, Australia

Wimbo wa Taifa wa Australia na kiapo cha uraia katika Kiswahili

Tume tafsiri Wimbo wa Taifa wa Australia na kiapo cha uraia katika lugha nyingi zinazo zungumzwa kote nchini Australia.

Published

By Gode Migerano
Presented by Gode Migerano
Source: SBS
SBS inawatambua wa Aboriginal na Watu kutoka Visiwa vya Torres Strait kote nchini Australia, kama Wamiliki wa Jadi wa Nchi, na uhusiano wao unao endelea kwa ardhi, maji na jumuiya.

Maandisi ya asili ya Advance Australia Fair, yali andikwa katika mwaka wa 1878 na mu Australia ambaye ni mwalimu na pia ni mwandishi wa nyimbo Peter Dodds McCormick. Wimbo huo ulithibitishwa kama wimbo wa taifa wa Australia tarehe 19 Aprili 1984.

Katika mwaka wa 2021 maneno katika mstari wa pili wa Wimbo wa taifa yalisasishwa kutoka ‘changa na huru’ nakuwa ‘mmoja na huru’ kumulika ujumuishi.

Wimbo wa taifa huchezwa katiak sherehe rasmi, mashindano ya michezo na matukio ya jumuiya.
Maneno ya Wimbo wa Taifa la Australia

Wa Australia sote tu furahie,
Kwa sababu tuna umoja na uhuru;
Tuna ardhi ya dhahabu na utajiri wakufanyia kazi;
Nchi yetu ime zungukwa na bahari;
Ardhi yetu imejaa zawadi za kiasili
Ya uzuri, utajiri na nadra;
Katika kurasa za historia, acha kila hatua
Australia iendelee.
Kwa sauti za furaha, tuimbe,
Australia iendelee.

Chini ya mwangaza wa mchoro wa Msalaba wetu wa Kusini
Tuta fanya kazi kwa mioyo na mikono;
Kufanya hii nchi yetu
Iwe maarufu zaidi ya nchi zote;
Kwa wale ambao wame kuja kwa bahari
Tuna nyanda zisizo na mipaka za kuchangia;
Tu ungane sote kwa ujasiri
Tu iendeleze Australia.
Kwa sauti ya furaha tuimbe,
Australia iendelee.
Australians Celebrate Australia Day As Debate Continues Over Changing The Date
- Credit: Don Arnold/Getty Images

Kiapo cha Uraia wa Australia

Tangu kuanzishwa kwa uraia wa Australia katika mwaka wa 1949, zaidi ya watu milioni sita wame kuwa raia kupitia utoaji rasmi wa uraia.

Sherehe za Uraia huandaliwa na halmashauri za jiji, pamoja na Siku ya Uraia ya Australia ambayo huadhimishwa tarehe 17 Septemba.

Kama sehemu ya sherehe, Wimbo wa Taifa ya Australia huchezwa, na watu hula kiapo kukubali wajibu wa uraia wa Australia.

Kuna aina mbili za viapo, aina moja ina mtaja Mungu.

Aina ya Kwanza ya Kiapo 

Kuanzia wakati huu, chini ya Mungu,
Na ahidi uaminifu wangu kwa Australia na watu wake,
ambao na changia imani zao zaki demokrasia,
ambao haki zao na uhuru, na heshimu, na
ambao sheria zake, nita shikilia na kutii.

Aina ya Pili ya Kiapo 

Kuanzia wakati huu,
Na ahidi uaminifu wangu kwa Australia na watu wake,
ambao na changia imani zao zaki demokrasia,

ambao haki zao na uhuru, na heshimu, na

ambao sheria zake, nita shikilia na kutii.

Soma na sikiliza Wimbo wa Taifa wa Australia na kiapo cha uraia katika lugha yako.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service