Serikali imeunga mkono nyongeza ya mshahara kwa wafanyakazi nchini wenye pato la chini, ikitoa uwasilishaji wayo kwa mapitio ya mwaka wa mishahara ya Tume ya kazi, kabla ya uamuzi wayo Juni.
Uwasilishaji wa serikali hauja toa pendekezo la kiwango cha nyongeza ya mshahara ila, ime hamasisha tume hiyo “ihakikishe mishahara halisi yawa Australia wenye pato la chini hairejei nyuma".
Hata hivyo, haija dokeza pia kuwa “mishahara yote inastahili ongezeka kulingana na mfumuko wa bei ", au kuwa mfumuko wa bei ndiyo sababu pekee ambayo Tume ya Haki kazini inastahili zingatia.
Chama kinacho wakilisha wafanyakazi A-C-T-U, kwa upande wacho kina weka shinikizo kwa ongezeko la kima cha chini cha mshahara wa 7%, pamoja na mishahara mingine kulingana na mfumuko wa bei.
Wakati Chumba cha Biashara na viwanda nchini Australia, kimependekeza ongezeko la kima cha chini cha 3.5% au 75c kwa saa, hadi $841.04 kwa wiki.