Watu wa asili kwenye hatihati ya kutoweka Brazil

Two officers with guns walking through an illegal mining camp in the Brazilian Amazon.

Officers of the Brazilian Institute of Environment and Renewable Natural Resources (IBAMA) take part in an operation against Amazon deforestation at an illegal mining camp, known as garimpo, at the Yanomami territory in Roraima State, Brazil, on February 24, 2023. - In early February Brazil deployed hundreds of police and soldiers to evict gold miners accused of causing a humanitarian crisis on the Yanomami Indigenous reservation, as thousands of the illegal miners fled. Justice Minister Flavio Dino said authorities estimate at least 15,000 people have illegally invaded the protected Amazon rainforest reservation, where Indigenous leaders accuse gold miners of raping and killing inhabitants, poisoning their water with mercury and triggering a food crisis by destroying the forest. (Photo by ALAN CHAVES / AFP) (Photo by ALAN CHAVES/AFP via Getty Images) Source: Getty, AFP / Alan Chaves

Shirika lisilo la faida linasema karibu nusu ya jamii za Wenyeji wanaoishi mbali na ulimwengu wanakabiliwa na kutoweka ndani ya muongo kutokana na ukataji miti, uchimbaji wa madini na utalii. Survival International wanasema wanataka ulimwengu - hususan serikali na viwanda - kutambua na kushughulikia tatizo hili kama dharura ya kimataifa.


Ndani ya misitu ya Amazon huko Brazil kuna eneo linalojulikana kama Bonde la Javari. Linajumuisha zaidi ya kilomita mraba elfu themanini na tano , na asilimia 99 ya msitu wake wa asili bado uko salama. Bonde hili ni nyumbani kwa yale ambayo Shirika la Kitaifa la Watu wa Asili la Brazil au FUNAI linasema ni mkusanyiko mkubwa zaidi wa makundi ya kiasili yasiyowasiliana katika Amazon - na duniani - wanaoishi kwa uwindaji, uvuvi, na kilimo kwa kiwango kidogo, wakidumisha lugha na mila ambazo zilikuwepo kabla ya taifa la kisasa.

Kwa miongo kadhaa Brazil ilihimiza mawasiliano na jamii hizi za kiasili ambazo zimetengwa - lakini ilibadilisha mkondo mwaka wa elfu moja mia tisa themanini na saba, ilikubali sera ya kutokuwepo mawasiliano, ambayo iliruhusu maingiliano endapo tu yatatokana na watu wa jamii za kiasili wenyewe.

 Vinginevyo, inapaswa waachwe pekee yao.

Shirika la Survival International linakadiria kuwa jumla kuna jumuiya mia moja tisini na sita kama hizo duniani kote, zilizotapakaa katika nchi kumi za Amerika Kusini, Asia, na Pasifiki, baadhi kama watu wa North Sentinel, wakishuhudia marufuku sawa.

 Shida ni kwamba watu hawa waliotengwa wanafinywa na barabara, wachimbaji madini na wafanyabiashara wa dawa za kulevya, mzozo unaofanyika mbali na macho ya umma au ulinzi wa serikali wenye ufanisi. Mkurugenzi mtendaji wa Survival International Caroline Pearce anasema wanakabiliwa na kutoweka ndani ya miaka kumi ijayo endapo hatua za dharura hazitachukuliwa.

tunahisi kwamba ni dharura kushughulikia swala hili - kufichua na kushughulikia hili - kama janga la kimataifa. Katika nchi zote kumi ambako watu wasio na mawasiliano wanaishi, wanashambuliwa hivi sasa.
Caroline Pearce
Survival International wamechapisha ripoti inayobainisha vitisho kwa jamii hizi zisizo na mawasiliano. Na ripoti ina takwimu za kusikitisha: inakadiriwa kuwa karibu asilimia sitini na tano ya watu wasio na mawasiliano wanakabiliwa na vitisho kutoka kwa uchimbaji wa misitu, takriban asilimia arubaini kutoka kwa uchimbaji madini na karibu asilimia ishirini kutoka kwa biashara ya kilimo.

 Caroline Pearce anasema kuwa unyonyaji mkubwa wa nikeli kukidhi mahitaji makubwa ya betri za magari ya umeme ni jambo la wasiwasi nchini Indonesia.

Kuna watu wa kabila la Hongana Manyawa ambao hawajawasiliana kwenye Kisiwa cha Halmahera nchini Indonesia, ambao wanawaonya wale wanaoboresha ardhi yao kwa uchimbaji wa nikeli. Tuna familia za kabila la Araya huko Paraguay ambazo kwa sasa zinakwepa wale wanaosafisha ardhi yao kwa ajili ya kufuga ng'ombe.
Caroline Pearce
Kwa jamii ya Kakataibo ya mkoa wa Ucayali nchini Peru, ni ukataji haramu wa miti na kilimo cha kakao. Mwanajamii wa Kakataibo, Herlin Odicio, haishi katika kutengwa na badala yake anapigania maslahi ya watu wake.

 
"Sisi kama mashirika ya Wenyeji tunafanya kazi kutetea haki zao za ardhi kwa sababu wao hawana watu ambao wanaweza kujitokeza na kupigania haki zao wenyewe. Wanapuuzwa na serikali. Serikali ya Peru inajaribu kuondoa sheria na kuanzisha sheria za kupinga Wenyeji ambazo zitakuwa mbaya sana kwa watu wasioguswa. Hii itamaanisha kuteketezwa kwa ndugu zetu ambao hawajaguswa
Herlin Odicio
Hoja ya Herlin ni kwamba si tu suala la kupoteza ardhi; pia kuna maisha yanayowekwa hatarini. Fiona Watson, mkurugenzi wa kampeni za Survival International, anasema kuwa wakati mwingine hilo linaweza kuchukua sura mbaya.

Mauaji ya kimbari ambayo tumeyaorodhesha na ambayo bado yanaendelea kadri tunavyojua ni yale ambayo ningeyaita mauaji ya kimya. Na hiyo ni kwa sababu hakuna timu za televisheni huko au waandishi wa habari wanaoripoti kwa sababu jamii zinazotengwa za wenyeji , wanaishi katika maeneo ya mbali sana yenye misitu kama Amazon au msitu wa mvua wa Indonesia na Papua Magharibi, na India.
Fiona Watson
Magonjwa ni hatari nyingine inayotishia watu ambao hawajaunganishwa na wengine.

Mnamo mwaka wa elfu mbili na ishirini, ugonjwa wa COVID ulienea kote ulimwenguni, na Brazil ilirekodi zaidi ya vifo 60 kutokana na virusi hivyo miongoni mwa watu wa kabila la Kayapo na makabila mengine.

Lakini mkurugenzi mkuu wa Baraza la Udhibiti wa Misitu, Subhra Bhattacharjee, anasema hata mafua ya kawaida yanaweza kuwa tishio.


[aridi rahisi ambayo mimi na wewe tunaweza kupona ndani ya wiki moja, ambayo mnaweza hata kwenda kazini ikiwa mnayo - wakiathiriwa, wanaweza kuuawa. Wanaweza kufa kwa baridi hiyo. Hawana kinga dhidi ya hiyo.
Subhra Bhattacharjee
Survival International inasema tishio hili mara nyingi halipewi kipaumbele na serikali, ambazo wakosoaji wanasema zinawaona watu wasioguswa kama wa pembeni kisiasa kwa sababu hawapigi kura na maeneo yao mara nyingi yanapigiwa upatu kwa ajili ya uvunaji wa miti, uchimbaji madini na uchimbaji mafuta.

Haki za kiasilia - hasa haki za ardhi - zinalindwa chini ya sheria za kimataifa - ingawa sheria za kitaifa zipo, NGO inasema utekelezaji mara nyingi ni dhaifu. Fiona Watson anasema wakati mwingine ni mamlaka yenyewe ndiyo inayohusika na miradi inayotishia."}

 
Bado kuna matatizo na miradi ya miundombinu. Kuna reli inayopangwa kuanzishwa nchini Brazil, katika eneo la Amazon, kusafirisha mazao ya kilimo kutoka kituo tajiri cha kilimo cha katikati ya magharibi, hadi kaskazini mashariki, na hivyo kuelekea Atlantiki ili kusafirisha mazao, jambo ambalo linaweza kuathiri watu wa kiasili watatu, ambao bado hawajawasiliana na watu wa nje
Fiona Watson
Kulingana na mwigizaji Richard Gere, ambaye amekuwa mwanaharakati wa muda mrefu na msaidizi wa shirika hilo, ukosefu wa kinga kali unadhihirisha jambo la kimsingi zaidi, ambapo upendeleo na mitazamo potofu vinaathiri mjadala wa umma.
Anasema kwamba upande mmoja, watu ambao hawajawasiliana na jamii za nje wanaweza kutazamwa kama "makabila yaliyopotea", ilhali upande mwingine, wanaonekana kama vizuizi kwa maendeleo.

Unajua, nilikulia katika nchi ambayo ilijengwa juu ya mateso ya watu wetu wa asili kule Amerika. Na ninayo aibu kubwa kuhusu hilo... Ilikuwa jambo lisilofaa kufanya na ilikuwa ukatili na haikuhitajika
Richard Gere

Herlin Odicio anasema uhifadhi wa watu ambao hawajawasiliana na wengine unahitaji sheria kali zaidi, na mabadiliko katika jinsi dunia inavyowaona.
Anasema kwamba wao sio mabaki ya zamani, bali ni raia wa sayari ambao maisha yao yanagusa mustakabali wa kila mtu.

Wana haki ya ardhi - haki juu ya maeneo ya mababu zao - lakini kuna shughuli haramu zinazoendelea katika maeneo hayo, uhalifu uliopangwa. Na hii inachangia ukosefu wa usalama na hatari wanayokabiliana nayo. Hatutaki serikali itufadhili. Hii ni haki tuliyokuwa nayo kwa miongo mingi.
Herlin Odicio


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service