Marita Tilleraas, anajua kwa uzito wa kwanza changamoto ya kulipia huduma za malezi ya watoto.
Ada za malezi ya watoto zimekuwa sawa na za mkopo wetu wa nyumba na zaidi. Kadri ninavyozidi kupata mshahara, kama nipate ongezeko la mishahara la asilimia 5 kwa sababu ya mfumuko wa bei, ada yangu ya malezi ya watoto itaongezeka kwa sababu katika kiwango kingine cha mapato ndipo ongezeko hilo la mshahara linapungua kwa sababu pesa zangu zote na zaidi huishia kwenye malezi ya watoto.Marita Tilleraas
Mama huyu wa watoto wawili anafanya kazi kwa muda wote na muda mrefu ameitaka "Activity Test" liondolewe, ni kipimo cha kustahiki kilichoanzishwa na Muungano tangu 2018 ambacho kinahitaji wazazi kufanya kazi, kusoma au kujitolea kwa saa fulani kwa wiki. Lengo la kuondoa jaribio hilo linashirikiwa na The Parenthood, shirika la utetezi ambalo pia linafanya kampeni ya kuweka mipaka kwenye ada za malezi ya watoto. Mkurugenzi wa Kampeni Maddy Butler anasema jaribio hilo limefanya maisha ya wazazi wengi kuwa magumu zaidi.
Tumekuwa tukisikia hadithi kwamba wazazi na walezi wamekuwa wakijaribu haraka kutafuta kazi za kujitolea ili waweze kupata huduma na elimu ya mapema, ili baadaye waweze - kwa muda zaidi - kutoka na kufanya kazi za kulipwa pia.Maddy Butler
Kuanzia wiki hii , serikali ya Albanese imehakikisha kuwa wazazi wanapata ruzuku ya asilimia 90 kwa siku tatu kwa wiki ya huduma ya watoto. Mhasibu Mkuu Jim Chalmers anasema kwamba hii itasaidia wazazi kote nchini.
Tunatarajia kama familia laki moja za Australia zitanufaika kutokana na dhamana ya siku tatu ya Serikali ya Leber ya Albanese. Sasa tunafanya kazi kwa misingi ya kwamba ikiwa ni nzuri kwa watoto, ikiwa ni nzuri kwa familia, ikiwa ni nzuri kwa mfumo wa elimu - basi pia ni nzuri kwa uchumi. Na ndiyo maana kama Mweka Hazina ninajivunia kweli kusaidia kupata fedha za dhamana hii ya siku tatu.Jim Chalmers
Serikali inasema kwamba siku hizi tatu hazitahitaji Jaribio la Shuguli ama Activity Test, hata hivyo jaribio hilo litatumika ikiwa wazazi wanataka kupata ruzuku ya utunzaji wa watoto kwa siku za ziada. Nesha Hutchinson, mmiliki wa kituo cha Cressy Road Early Learning, anasema kuondoa jaribio kwa siku hizi tatu ni hatua nzuri ya kwanza ili kufanya huduma hii ipatikane kwa urahisi zaidi kwa wazazi.
Tumekuwa na familia ambazo zimekuwa na watoto wanne kwa wakati mmoja chini ya uangalizi wetu, jambo hili sio la bei rahisi. Kukomesha hili kunamaanisha kwamba hawatahitaji kufanya mahesabu haya mara nyingi na wanaweza kufanya maamuzi kwa kuzingatia maslahi bora ya familia, ya familia yao wenyewe, na ya watoto wao.Nesha Hutchinson
Mkurugenzi wa Kampeni wa Parenthood, Maddy Butler, anasema ruzuku hizi kutoka serikalini hazitasaidia kuondoa tatizo la gharama peke yake.
Wakati wowote nyongeza hizi za ruzuku zinapotolewa, mara nyingi zimefuatiwa na ongezeko la ada kutoka kwa watoa huduma wengi. Ndiyo sababu tunaiomba Serikali ya Shirikisho kutengeneza modeli ya ada inayofungwa, ili kufanyia marekebisho mfumo na kuhakikisha kuwa ni rahisi kwa familia kutumiaMaddy Butler
Lakini ruzuku ya Uangalizi wa Watoto haitoi uhakika wa kujiunga na mtoa huduma yeyote. Familia bado zitahitaji kupata nafasi kwa huduma ya uangalizi wa watoto waliochagua, na huenda zikahitaji kulipa ada ya tofauti. Mama wa watoto wawili Jen Fleming anasema imekuwa vigumu sana kumpatia binti yake nafasi katika kituo cha uangalizi wa watoto.
Niliweka jina la binti yangu ya kwanza wakati nilikuwa na ujauzito wa wiki 20. Sasa ana miaka minne na nusu na bado hajapewa nafasi katika kituo hicho.Jen Fleming
Baada ya kupitia changamoto hii, Bi. Fleming ameendelea kutetea kwamba ruzuku mpya ya serikali itoe pia msaada kwa njia mbadala za malezi ya watoto
Inaweza kuwa yaya au babu na nyanya, inaweza kuwa mkufunzi wa vijana wa kigeni, inaweza kuwa sehemu ya kufanya kazi pamoja inayoiruhusu mama kurudi kazini mapema, lakini aendelee kunyonyesha. Inahitajika kuwa na upanuzi wa mfumo kutambua aina zote za malezi.Jen Fleming
Kiongozi wa Upinzani Susan Ley anasema ruzuku hizo hazitatui suala la uhaba wa chaguo za huduma za watoto na kuondoa mtihani kunaweza kufanya mambo kuwa magumu zaidi kwa baadhi ya wazazi wanaofanya kazi.
Pengine mnaweza kupata familia katika kila eneo la msimbo wa posta ambazo haziwezi kupata nafasi ya siku moja. Jambo lingine linalotusumbua ni kuondoa kipimo cha shughuli na hii inamaanisha kuwa watu wanaofanya kazi au kusoma hawapati kipaumbele tena, na siku zote tuliamini kuwa familia hizo zinapaswa kuwa na kipaumbele katika malezi ya watoto.Susan Ley







