Key Points
- Return home only when authorities say it’s safe and take precautions like checking for lingering embers.
- Recovery centres, financial assistance and mental health services are available to help you navigate the practical and emotional impacts of bushfires.
- Bushfire recovery takes time, and leaning on community support and caring for your wellbeing is essential.
- Ni lini ni salama kurejea nyumbani baada ya moto wa vichaka?
- Ni tahadhari gani unapashwa chukua, unapo rejea katika nyumba iliyo athiriwa kwa moto?
- Ni vituo gani vya uokoaji na usaidizi wa kifedha unao patikana baada ya moto wa vichaka?
- Moshi wa moto wavichaka unaweza athiri aje afya yako?
- Unaweza pata wapi msaada wa afya ya akili baada ya moto wa vichaka?
- Wazazi wanawezaje wasaidia watoto na vijana baada ya janga?
- Umuhimu wa msaada wa jamii ni nini wakati wa uponaji wa moto wa vichaka?
Unaweza hisi unalemewa wakati wa kupona kutokana na moto wa vichaka, hata hivyo msaada unaweza patikana. Kuanzia kurudi salama nyumbani, hadi kusaidia kwa afya na ustawi wako, hizi ndizo hatua muhimu za kuchukua baada ya tukio la moto wa vichaka.
Ni lini ni salama kurudi nyumbani baada ya tukio la moto wa vichaka?
Waaustralia hukumbushwa mara kwa mara kuhusu umuhimu wa kuwa na mpango wa moto wa vichaka. Ila, nini kitatokea baada ya moto huo kuisha?
Ikiwa umehama, rudi nyumbani tu Huduma yako ya Dharura ya Jimbo (SES) inapokuambia ni salama kufanya hivyo. Kurudi mapema sana kunaweza kuweka katika hatari ya miundo isiyo imara, nyaya za umeme zilizoanguka au sehemu zenye joto kali.

Unastahili fanya nini unaporudi katika nyumba iliyo athiriwa kwa moto?
Unapo ruhusiwa kurudi nyumbani, leta vitu muhimu kama vile chakula kisichoharibika, maji ya chupa, pesa taslimu, tochi na betri za ziada.
Kama nyumba yako bado imesimama, anza kwa kuangalia uharibifu unao onekana wa kimuundo kabla ya kuingia ndani. Unapoingia katika nyumba iliyoathiriwa na moto, vaa kifaa cha kupumua, glavu, vazi la mikono mirefu na viatu vyenye kinga nzuri. Ikiwezekana, hifadhi watoto na wanyama wa nyumbani sehemu salama kwanza.
Tafuta kwa makini makaa yanayowaka, kwa sababu yanaweza waka tena siku chache baada ya moto mkuu kupita.
Sharif Baytieh, ni naibu nahodha wa kikosi cha Huduma ya Zimamoto Vijijini katika kijiji cha Nana Glen jimboni New South Wales, ameona hili hiyo ikitokea mara nyingi. Kote nchini Australia, zaidi ya wazima moto 100,000 wa kujitolea kama Sharif huelimisha jamii, hupambana na moto na kusaidia katika shughuli za uokoaji. Alikabiliana na moto wake mkubwa wa kwanza wa vichakani katika mwaka wa 2019.
“Tulipokea wito kila mara baada ya moto kwa takriban wiki mbili, na ilikuwa mmiliki wa mali ambaye angekuwa na gogo ambalo hakugundua bado lilikuwa linawaka, na likitoa moshi,” anakumbuka. “Tulikuwa na upepo fulani siku saba hadi nane baadaye ambao uliwasha vitu hivi na jambo linalofuata unajua, wanaangalia dirisha lao la nyuma na kuna gogo linawaka moto. Makaa hayo na sehemu hizo za moto, zinaweza kuwasha moto, haswa ikiwa ziko karibu na nyumba yako..”
Ni vituo gani vya uponaji na misaada yakifedha hutolewa baada ya moto wa vichaka?
Makao ya dharura na vituo vya usaidizi vimeanzishwa kwa ajili yakutoa usalama na usaidizi wa haraka. Kwa kawaida huwa wanatoa malazi, chakula, maji na vituo vya kuchaji, na pia wanaweza kuwa na washauri na huduma za rufaa zinazohusu majeraha.
Huduma za serikali kama vile Emergency Recovery Victoria, Service NSW au Queensland Recovery Hotline zinaweza wasaidia watu kukabiliana na kile kinachofuata.
Msaada wa kifedha wa serikali wakati wa maafa unaweza patikana pia, kulingana na hali yako.
Kama una bima, andika kila kitu kabla ya kuhama au kusafisha chochote. Piga picha na video na uweke rekodi iliyoandikwa ya hasara. Baadhi ya makampuni ya bima hutoa malipo ya haraka kwa vitu muhimu kama vile malazi ya muda.

Moshi wa moto wa vichaka unaweza athiri aje afya yako?
Moshi wa moto wa vichaka huathiri watu walio karibu na mbali na moto, na huathiri ubora wa hewa, afya na maisha ya kila siku. Watu wanaoishi na matatizo ya moyo au kupumua wako katika hatari kubwa zaidi.
Daktari wa dharura na mtaalamu wa afya ya umma na majanga Dkt. Lai Heng Foong, amesema athari hizo zinaweza kudumu kwa muda mrefu baada ya moshi kuisha.
"Kama tulivyoona katika moto wa vichaka wa Black Summer, kukaa muda mrefu kwenye jua kunaweza kuathiri ukuaji wa watoto ambao hawajazaliwa. Inachangia magonjwa ya moyo, shida ya akili, saratani, kiharusi, kisukari na tusisahau, afya mbaya ya akili," anasema.
Unaweza pata wapi msaada wa afya ya akili baada ya moto wa vichaka?
Athari za afya ya akili za majanga yanayojirudia zinaweza kuwa kubwa, hasa kadri mabadiliko ya hali ya hewa yanavyoongeza marudio na ukali wa moto wa vichaka.
“Na inapokuja mara kwa mara, ambayo tutaona katika siku zijazo kwa sababu mabadiliko ya hali ya hewa husababisha athari kubwa zaidi kwenye matukio ya maafa, na kuifanya iwe ya mara kwa mara na pia kuwa makali zaidi, na kila wakati inapotokea, watu huchochewa na uzoefu huo, wana hatari kubwa ya wasiwasi na mfadhaiko na athari zote za msongo wa mawazo baada ya kiwewe,” Dkt. Lai anasema.
Usaidizi unapatikana kupitia vituo vya kupona, daktari wako wa familia, na simu za usaidizi za saa 24/7 kama vile Lifeline au Beyond Blue.

Wazazi wanawezaje wasaidia watoto na vijana baada ya janga?
Kuwasaidia watoto na vijana baada ya janga ni muhimu. Ustawi wa mzazi una jukumu kubwa kwa jinsi watoto wanavyokabiliana na hali zao.
Erin Pelly, ni meneja wa kitaifa wa huduma za kupona na dharura wa Msalaba Mwekundu nchini Australia, amwsema malezi baada ya janga yanaweza kuwa mgumu sana.
“Kulea watoto baada ya janga ni jambo gumu sana. Kuna mambo mengi tofauti ya kukabili. Watoto wako wanaweza kuwa wanapitia hisia na mawazo au athari zinazofanana au zenye changamoto kwa janga hilo. Hilo ni jambo la kawaida sana. Nyote mmepitia mengi, kwa hivyo kuwatuliza na kuwapa utunzaji na faraja labda ndilo jambo muhimu zaidi unaloweza kufanya. Hakuna anayemjua mtoto wako kama wewe unavyomjua.”
Ukigundua tabia inayo leta wasiwasi kwa mtoto wako, tafuta msaada mapema kupitia daktari wako wa familia au simu ya usaidizi. Simu ya Usaidizi kwa Watoto hutoa ushauri wa siri kwa simu na mtandaoni kwa vijana wenye umri wa miaka mitano hadi 25.
Ni kwa nini msaada wa jamii ni muhimu sana kwa uponaji wa moto wa vichaka?
Uponaji huonekana tofauti kwa kila mtu na mara nyingi huchukua muda mrefu kuliko watu wanavyotarajia.
Erin Pelly amewahimiza watu kutenga muda kwa ajili ya muda mfupi wa furaha wakati wa kupona, iwe ni kutengeneza kikombe cha chai, kwenda kutembea na familia au kuandaa kuchangia chakula na majirani.
Ukiwa na uwezo wa kuwasaidia wengine, si lazima iwe jambo kubwa. Kuwepo tu kunaweza leta tofauti kubwa.
"Kujua kwamba kuna mtu anayejali, kujua kwamba kuna mtu anayesikiliza unachopitia na kukusaidia kukubali kilichotokea, ni muhimu sana kwa watu. Kwa hivyo, si lazima iwe kuchangia vitu au kutoa pesa au kutoa muda bali kuchangia moyo wako na mtu unayemsikiliza," amesema.
Kupona kutokana na moto wa vichaka ni safari ndefu, lakini msaada unapatikana kwa usalama wako, nyumba yako na ustawi wako.
Jiandikishe au fuata makala yaliyo rekodiwa ya Australia Fafanuliwa kwa taarifa na vidokezo muhimu zaidi kuhusu kuanza maisha yako mapya nchini Australia.
Je, una maswali yoyote au mawazo ya mada? Barua pepe: australiaexplained@sbs.com.au









