Ripoti ya kwanza ya kitaifa kuhusu ubaguzi wa rangi katika vyuo vikuu nchini Australia imegundua kuwa ni tatizo lililo enea na la kimfumo.
Ripoti hiyo iligundua kuwa asilimia 70 ya wanafunzi na wafanyakazi kutoka vyuo vikuu 42 walishuhudia ubaguzi wa rangi.
Viwango vya ubaguzi wa rangi vilikuwa juu zaidi miongoni mwa wanafunzi na wafanyakazi wa Asili, Wachina, Waafrika, Wayahudi na wanafunzi kutoka Mashariki ya Kati; wakati asilimia sita pekee ya waliopitia uzoefu wa ubaguzi wa rangi waki wasilisha malalamishi.
Kikosi Kazi cha Serikali cha Elimu ya kupambana na ubaguzi wa Wayahudi kinatarajiwa kuwafahamisha mawaziri wa elimu siku ya Ijumaa [[20 Feb]] kuhusu mabadiliko ya mafunzo ya walimu ili kupambana na ubaguzi wa rangi.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.





