Ofisi ya Hali ya Hewa imetoa maonyo makali ya hali ya hewa kwa kaskazini magharibi mwa New South Wales, sehemu za kati na kaskazini mwa Victoria, kaskazini mashariki mwa Australia Kusini, na kusini magharibi mwa Queensland - huku mvua kubwa ikinyesha na hatari ya mafuriko ya ghafla ikiongezeka. Sehemu za kaskazini-mashariki mwa Kusini Australia na kaskazini-magharibi mwa New South Wales, zinatarajiwa kupokea hadi milimita 300 ya mvua katika siku zijazo.
Seneta wa chama cha Greens David Shoebridge ametoa wito kwa watoto na wake wa wa Australia waliokuwa wapiganaji wa kundi la I-S, waliokufa au waliofungwa kurejeshwa nyumbani, wakati Upinzani wa Mseto una ongeza juhudi za kuwazuia kurejea nchini.
Seneta Shoebridge ameongezea kuwa, vyama vikuu vina tumia mbinu mbaya na amesema kurejea kwa utaratibu kwa raia 34 waliokwama Syria ndio jibu bora.
Serikali ya Sudan inayoungwa mkono na jeshi imekosoa UIganda kwa kumkaribisha mkuu wa wanamgambo wa RSF Mohamed Hamdan Daglo maarufu kama Hemeti. Hemeti alikutana na Rais Yoweri Museveni katika Ikulu ya Entebbe Ijumaa.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.





