Wanariadha kutoka nchi mbalimbali walijumuika mjini Bathurst tarehe 18 Februari 2023, kuwania taji kadhaa za riadha.
Kama ilivyo desturi wakenya waliwasili kwa kishindo nakuwaacha washindani wao wakiona visigino vyao, walipokuwa waki elekea kunyakua medali moja baada ya nyingine.
Allan ni mkaaji wa jiji la Bathurst, na katika mazungumzo maalum na SBS Swahili aliweka wazi fahari aliyopata kushuhudia mashindano hayo anako ishi pamoja na heshima anayo pata jijini humo baada yamatokeo chanya ya wanariadha wa Kenya.