Hiyo ni wastan ya kila 10 za nguo kwa kila mtu. Hata hivyo, tuki chagua kuchakata, kuchangia au kabadilisha na wengine nguo ambazo hatutaki, tunaweza saidia kukabiliana na mgogoro wa taka za nguo.
Sekta ya mitindo ni moja ya sekta kubwa ya uchafuzi wa mazingira.
Baraza la mitindo la Australia limeripoti kuwa kwa wastan, huwa tuna nunua nguo mpya 56 kila mwaka.
Mitindo ya kasi niya bei nafuu, ni nguo ambazo hazi valiwi sana na huzalishwa kwa wingi kwa ajili yaku endana na mahitaji ya muda. Hii ime undwa kuwa hamasisha wateja kununua mara kwa mara mavazi mapya, kwa maana kuwa tuna nunua nguo nyingi haraka na zinavaliwa, zina haribika au zinachokwa.
Ni jukumu letu kutupa nguo zetu katika hali yaku wajibika. Hii inamaana kuhakikisha nguo hizo hazi ishii katika jalala na badala yake, kufanya mipango ya nguo hizo kutumiwa tena au kutengezwa upwa.
Kama unataka shiriki katika hafla zakubadilishana mavazi, bonyeza hapa: www.clothingexchange.com.au