Mapema mwezi huu, serikali ya shirikisho ilipitisha muswada wake wa makato ya kodi kwa ma milioni ya wafanyakazi nchini Australia, iliyo ahidiwa katika kikao cha wiki ya kwanza tangu uchaguzi mkuu wa Mei.
Katika wiki mbili zilizo pita, wanasiasa wa shirikisho wamekuwa wakijumuika na wapiga kura katika maeneo bunge yao. Hata hivyo serikali haija pata mapumziko yoyote wiki hii...
Wiki yakisiasa nchini ilikamilika kwa mkutano kati ya waziri mkuu na waziri wa NZ, Jacinda Ardern mjini Melbourne.
Huo ni mkutano wao kwa kwanza, tangu Bw Morrison alipoenda New Zealand kutoa heshima zake, kwa waathiriwa wa shambulizi laki gaidi mjini Christchurch.
Share






