Jeshi la polisi lilipokuwa liki kabiliana na baadhi ya waandamanaji katika upande mmoja wa jiji la Nairobi, kundi la watu wasio julikana walikuwa wakivamia nakupora mifugo na mali katika shamba la Rais mstaafu Uhuru Kenyatta ambalo liko nje ya Nairobi bila polisi kuingilia kati.
Hali hiyo imezua maswali kuhusu utendaji wa jeshi la polisi la Kenya, ambapo baadhi yawatu wanahisi hatua zinachukuliwa kutegemea na mrengo wakisiasa ambao watu wanafuata.
SBS Swahili ilizungumza na mchambuzi wa maswala ya usalama nchini Kenya na Afrika Mashariki, Bw George Musamali kuhusu hali inavyo endelea nchini Kenya. Bonyeza hapo juu kwa mahojiano kamili.