Matukio ya hali ya hewa kama mafuriko, mioto ya vichaka, dhoruba na vimbunga, ni sehemu ya kawaida ya maisha katika sehemu nyingi za Australia. Na hata kama una kodi nyumba, bado unaweza athiriwa na vitu kama uharibifu wa maji au wezi.
Katika makala haya ya Australia ya Fafanuliwa, watalaama wetu wata chambua mambo muhimu ya bima ya nyumba na yaliyomo, ikiwa ni pamoja na kutengwa kwa kawaida, vitu muhimu vyaku tilia umakini na unachoweza fanya kuhusu ongezeko ya malipo.
Iwapo una miliki nyumba yako au unapanga, bima ya nyumba ni kitu unastashili zingatia.
Jisajili au fuata makala yaliyo rekodiwa ya Australia ya fafanuliwa, kwa habari muhimu zaidi na vidokezo kuhusu kuanza maisha yako mapya nchini Australia.
Una swali lolote au wazo la mada? Tutumie barua pepe kwa: australiaexplained@sbs.com.au