Katika makala haya, tuta chunguza kwa nini ni muhimu kuwa makini na kuwa na heshima, ya maadili ya asili naya kitamaduni ya sehemu hiyo, unapo panga kwenda nje kutembea katika jangwa la Australia.
Hii ina maana kubaki katika barabara na njia maalum, kufuata mwongonza na ushauri, kuto tupa taka au kuharibu mandhari na kuto ondoa mimea ya asili au wanyama.
Unapo tembelea mbuga zakitaifa na sehemu zingine za nyika kote nchini Australia, kuna aina nyingi ya mimea, wanyama na mandhari yakutembelea nakufurahia.
Jiandikishe au fuata makala yaliyo rekodiwa ya Australia Explained kwa taarifa za ziada na maelezo muhimu kuhusu kuanza maisha yako mapya nchini Australia.
Una maswali yoyote au mawazo ya mada? tutumie barua pepe kwa australiaexplained@sbs.com.au