Makala:Serikali ya Victoria kuendelea na ubomozi wa nyumba za umma licha ya upinzani

Katika wakati wa mgogoro wa makazi na gharama za maisha, serikali ya Victoria iko katika mchakato wa kubomoa minara yote 44 ya makazi ya umma ya Melbourne. Licha ya upinzani mkubwa na uchunguzi wa bunge unaotaka kusitishwa kwa haraka kwa kazi hizo, serikali ya Victoria inaendelea na mipango hiyo. Kuhama nyumba huchukuliwa kuwa moja ya matukio yenye msongo mkubwa zaidi katika maisha ya mtu. Kwa hivyo, mwaka 2023, wakati maelfu ya wakaazi wa Victoria walipokea taarifa kwamba nyumba zao zitabomolewa wakati fulani kati ya mwaka huo na 2051, msongo ulikuwa dhahiri. Tembelea tovuti yetu sbs.com.au kwa taarifa ama maelezo zaidi.
Share



