Jamii mbali mbali zawa Afrika zinazo ishi Australia, zina makanisa yao ambako huwa wanajumuika kwa ibada, na isitoshe kuna vikundi vidogo vidogo vya waumini ambavyo huanza kanisa zao binafsi.
Hata kama lengo na shabaha ni moja ya wachungaji wanao ongoza makanisa hayo, ni nadra kwa wachungaji hao kuungana nakuandaa tukio linalo jumuisha makanisa mengine.
Ila, wikendi iliyopita baadhi ya wachungaji wenye asili ya ukanda wa Afrika ya Kati walijiunga nakuandaa kongamano maalum mjini Sydney. SBS Swahili ilizungumza na Mchungaji Joseph Mucunda, aliyezungumza kwa niaba ya wachungaji wenzake walio andaa kongamano hilo.