Ila baada ya vizuizi na marufuku ya watu wengi kukutana kuondolewa, ma promota kote nchini wamerejea sokoni kuandaa tamasha mbali mbali ambazo zime leta watu pamoja tena.

Mejja awapa mashabiki wake tiba Source: Sam K
Sam ni mkurugenzi wa kampuni ya Melbourne Party Rockers, kampuni hiyo kwa ushirikiano na Adelaide Reloaded wame mleta msanii maarufu na mashuhuri kutoka Kenya, Mejja "Okonkwo" kwa tamasha katika miji mitano mikubwa ya Australia. Bw Sam alieleza SBS Swahili jinsi wapenzi wa muziki walivyo mpokea kipenzi chao, pamoja na maandalizi ya tamasha zingine kuelekea mwisho wa mwaka huu.