Tofauti na wasanii wenza ambao hutilia maanani kazi zao kimziki tu, msanii huyo wa hip hop kutoka Kenya ana shirika lamisaada (Octopizzo Foundation) linalo wasaidia vijana katika meaneo ya Kibera aliko kuia. Shirika hilo hutoa huduma pia katika sehemu zingine nchini Kenya.
SBS Swahili ilizungumza na Octopizzo, alipokuwa katika ziara kusini Australia, ambako alishiriki katika tamasha ya kila mwaka maarufu kwa jina la Sanaa Festival mjini Adelaide, pamoja nakushiriki katika jopo aliko zungumza kuhusu kazi ya shirika lake la misaada la Octopizzo Foundation.
Bofya hapo chini kwa taarifa ya ziada, kuhusu kazi ya shirika la Octopizzo Foundation.
octopizzofoundation.org