Taarifa ya Habari 11 Februari 2025

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Kundi maarufu la madaktari limezindua mpango mpya kabla ya uchaguzi mkuu, kundi hilo limesema lita hakikisha upatikanaji kwa huduma yama GP kwa bei nafuu kwa kila mtu nchini Australia.


Mjadala kuhusu viza za wahamiaji matajiri ume fufuka baada ya serikali ya New Zealand kutangaza, kuwasilishwa kwa mfumo wa tiketi ya dhahabu. Wawekezaji matajiri watahitaji ishi kwa muda wa siku 21 nchini New Zealand, kwa muda wa miaka mitatu ili wapate makazi yakudumu.

Mshauri wa maswala ya kifedha wa waAustralia wa kwanza amesema mpango wa serikali waku weka vikomo kwa gharama ya vyakula muhimu, inaweza saidia kuboresha afya ya jumuiya yawa Australia wa kwanza katika vijiji vya Australia. Waziri Mkuu ame weka wazi kikomo hicho baada yakuthibitishwa kuwa ni pendekezo 5 tu kati ya 19 ya malengo yakufunga pengo, ambayo yametimizwa.

Hali ya utulivu wa mashaka inashudiwa mashariki mwa DR Kongo baada ya viongozi wa kikanda wenye hofu ya vita vikubwa zaidi kutoa wito kwa vikosi vya Kongo na vile vinavyoungwa mkono na Rwanda kusitisha mapigano.

Sam Nujoma ambaye aliongoza mapambano ya miongo mitatu ya kupigania uhuru wa Namibia kutokea Afrika Kusini yenye ubaguzi wa rangi, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 95, ofisi ya rais ilitangaza Jumapili.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa ya Habari 11 Februari 2025 | SBS Swahili