Mbunge anaye wakilisha jamii ya kijiji cha Burketown ambacho kiko katika eneo la kaskazini magharibi Queensland, amesema ni mhimu misaada yote itolewe kuwasiaida wakaazi wanao kabiliana na kilele cha mafuriko na uponaji. Idadi kubwa ya wakaaji 150 wa kijiji hicho, wame hamishwa kwa helikopta na ndege nakupelekwa katika vijiji jirani. Mto Albert tayari umepitisha mita saba na, ulitarajiwa kupitisha kilele chake leo jumapili 12 Machi. Kiwango hicho ni zaidi ya rekodi ya mafuriko ya mita 6.78 iliyowekwa katika mwaka wa 2011.
Ndege ya mizigo iliyobeba mahema, vifaa vya afya, na misaada mingine ya kibinadamu ilitua siku ya Ijumaa katika mji wa mashariki wa Goma huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Huu ni msaada wa kwanza kupelekwa huko chini ya mpango wa Umoja wa Ulaya (EU) ili kuwasaidia mamilioni ya watu waliokoseshwa makazi katika eneo hilo. Mapigano kati ya jeshi la Kongo na M23, kundi la waasi ambalo linadai kuwakilisha maslahi ya watu wa kabila la Watutsi walioko mashariki mwa Congo. Mapigano hayo yamesababisha ongezeko la mzozo wa kibinadamu huku zaidi ya watu milioni 5.5 wakikoseshwa makazi katika majimbo kadhaa.
Waalimu katika shule za serikali nchini Sudan wamekuwa kwenye mgomo tangu Novemba kutokana na mishahara midogo na kutolipwa ujira wao. Wanaishutumu serikali ya kijeshi kwa kushindwa kuweka kipaumbele kwenye elimu na wanataka kurejeshwa kwa serikali ya kiraia. Wakati huo huo, waziri wa fedha wa Sudan anasema serikali imekidhi madai ya waalimu. Shule hazina wanafunzi ambao ni kawaida kuonekana kote nchini Sudan. Tangu Novemba, waalimu wameitisha migomo kadhaa, wakipinga mishahara kwamba katika baadhi ya kesi hawalipwi kwa miezi kadhaa, na waalimu wanasema ni midogo mno.