Taarifa ya Habari 13 Juni 2025

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Balozi wa zamani wa Australia nchini Marekani, Arthur Sinodinos, amesema mkataba wa AUKUS unastahili kuwa kipaumbele kikuu katika mkutano kati ya Waziri Mkuu Anthony Albanese na Rais wa Marekani Donald Trump.


Wakaaji wa Tasmania wamesema wana hisa mseto kuhusu kupiga kura katika uchaguzi mwingine wa jimbo hilo. Ombi la uchaguzi wa mapema la kiongozi wa jimbo hilo na kiongozi wa chama cha Liberal, Jeremy Rockliff lilikubaliwa na gavana wa jimbo hilo usiku wa Jumatano 11 Juni, siku sita baada yakupoteza kura ya kutokuwa na imani dhidi ya uongozi wake bungeni.

Mwanaharakati wa ulemavu wa Queensland amekosoa sheria za uhalifu wa vijana jimboni humo, katika hotuba yake kwa Umoja wa Mataifa mjini New York. Mwana sheria wa haki za binadam Tom Dixon kutoka shirika la Queensland Advocacy for Inclusion group ame eleza Umoja wa Mataifa kuwa, uwakilishi mkubwa wa watoto wenye ulemavu katika magereza ya Queensland ni ishara wazi kuwa mfumo wa haki wa uhalifu umevunjika.

Utata unaendelea kutanda nchini Kenya kufuatia kifo cha Albert Ojwang, mwanamume mwenye umri wa miaka 31 aliyekamatwa Jumamosi, Juni 7, na ambaye alifariki usiku uliofuata akiwa kizuizini. Wakati matokeo ya uchunguzi wa maiti uliofanyika Jumanne, Juni 10, kwenye mwili wa mwathiriwa yalipingana na toleo la awali la polisi kwamba aligonga kichwa chake kwenye ukuta wa chumba alikokuwa anazuiliwa—badala yake, yamerejelea majeraha “yaliyosababishwa na kitu alichopigwa kutoka nje,” yakibainisha kwamba alikuwa mlengwa wa shambuli - watu wameendelea kutoa hisia zao kote nchini.

Siku sita baada ya uchaguzi uliopingwa wa Juni 5 ambapo Warundi walichagua wabunge wao na madiwani wa manispaa, Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi (CENI) imetangaza matokeo ya muda ya uchaguzi huo wa wabunge wakati wa sherehe rasmi mjini Bujumbura Jumatano, Juni 11. CNDD-FDD, chama ambacho kimeitawala Burundi kwa mkono wa chuma tangu mwaka 2005, ndicho kimeibuka mshindi kwa zaidi ya 96% ya kura zilizopigwa. Vyama vingine 20 vya kisiasa na miungano iliyoingia kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi, hata hivyo, wanasema uchaguzi huo uliibiwa, na hakuna aliyepata zaidi ya 1% ya kura, isipokuwa chama cha zamani cha Uprona, kilichoshika nafasi ya pili kwa 1.3% ya kura.


Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service
Taarifa ya Habari 13 Juni 2025 | SBS Swahili