Chama cha Liberal cha NSW kime lazimishwa kumtema mmoja wa wagombea wao chini ya wiki mbili kabla ya uchaguzi wa NSW, wakati mgombea mwingine amejipata hatarini kwa madai aliyotoa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa. Mgombea wa chama cha Liberal wa eneo bunge la Wyong ambalo liko katika kanda ya Central Coast, alivuliwa ugombea wa chama kwa sababu ya machapisho yakukera katika mtandao wa jamii ambayo yalijumuisha madai yakukera kuhusu wapenzi wa jinsia moja, Uislamu na chanjo.
Utafiti wamajaribio kutoka chuo cha Griffith cha Queensland, umepata viungo kati ya madhara ya Uviko wa muda mrefu na ugonjwa wa uchovu sugu kwenye ubongo.
Makamu wa Rais Kamala Harris atafanya ziara ya wiki moja barani Afrika mwishoni mwa Machi huku Marekani ikiongeza mawasiliano yake kwa bara hilo huku kukiwa na ushindani wa kimataifa, haswa na China. Bi Harris atafanya ziara Ghana kuanzia Machi 26 hadi 29, kisha Tanzania kuanzia Machi 29 hadi 31. Na kituo chake cha mwisho kitakuwa Zambia Machi 31 na Aprili mosi.
Watu wapatao 11 wamekufa katika mji wa Blantyre, Malawi na wengine 16 hawajulikani walipo baada ya kimbunga Freddy kuikumba nchi hiyo mwishoni mwa juma. Msemaji wa polisi ya Malawi, Peter Kalaya ameliambia shirika la habari la Reuters kwamba timu ya uokozi inawatafuta watu katika vitongoji vya Chilobwe na Ndirande, ambavyo vimeathiriwa vibaya.