Rais wa Marekani Donald Trump amesema serikali yake haija husika katika mashambulizi ya Israel dhidi ya Iran siku ya Ijumaa 13 Juni. Mwana diplomasia mkuu wa Iran Abbas Araghchi, amesema Iran ina ushahidi thabiti kuwa vikosi vya Marekani vili isaidia Israel katika mashambulizi yake.
Udhibiti wa sekta ya malezi ya watoto uta imarishwa, na hatua za lazima zita anza kutekelezwa kuanzia Septemba mosi. Mageuzi hayo yame afikiwa na mawaziri wa elimu kutoka majimbo na wilaya zote za Australia.
Walimu katika Kaunti ya Kisumu wameapa kugoma kuanzia Jumatatu wakitaka Naibu Mkuu wa Polisi, Eliud Lagat, ajiuzulu kufuatia kifo cha mwalimu na mwanablogu Albert Ojwang’.
Ulinzi ume endelea kuimarishwa katika kanisa la Askofu Gwajima, hatua ambayo ime walazimishwa waumini kufanyia ibada barabarani.