Waziri wa mambo ya nje Penny Wong, amesema serikali ya Australia inafanya iwezavyo, kuwasiadia wa Australia ambao wamekwama katika vita kati ya Israel na Iran. Amesema wa Australia 350 nchini Iran na wengine 300 nchini Israel, wamesajili ombi laku ondolewa katika Idara ya mambo ya kigeni na biashara. Idadi ya vifo nchini Iran imeongezeka hadi 224, ikijumuisha wanawake 70 pamoja na watoto, wakati wa Israeli 17 wame uawa tangu uhasama huo kuana siku nne zilizopita.
Shirika la msaada jimboni Queensland lina tumai kuongeza upatikanaji kwa michezo kwa wa Australia wenye ulemavu. Utafiti wa hivi karibuni umeonesha kuwa watu wenye ulemavu hupokea mafao sawia kwa kushiriki katika michezo na shughuli zakimwili kama wale ambao hawana ulemavu.
Kiongozi wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania, Tundu Lissu, anayekabiliwa na kesi ya uhaini, ameiambia mahakama hii leo Jumatatu kwamba amenyimwa haki yake ya msingi ya kisheria na kwa hivyo atasimama kujitetea mwenyewe kwenye kesi hiyo inayobeba adhabu ya kifo ikiwa atakutwa na hatia.
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, amesaini sheria inayoruhusu mahakama za kijeshi nchini humo kuendesha kesi za kiraia. Hayo yameelezwa na bunge la nchi hiyo leo, katika hatua ambayo viongozi wa upinzani wamesema inakiuka uamuzi uliotolewa na mahakama ya juu.