Taarifa ya Habari 17 Machi 2025

Bench - Swahili.jpg

Waziri Mkuu na kiongozi wa zamani wa chama cha Liberals Malcolm Turnbull, amesema hadhani Australia inastahili endelea mbele na ushirikiano wa AUKUS, ametoa maoni hayo wakati wasiwasi una ongezeka iwapo mkataba huo uta tekelezwa chini ya muhula wa pili wa uongozi wa Trump.


Waziri wa Ulinzi wa Marekani Pete Hegseth mwezi ulio pita alisema rais ana unga mkono mkataba huo wenye thamani ya dola bilioni 368, baada ya Australia kulipa milioni 800 kwa mpango wakupata manowari yanayo tumia nishati ya nyuklia. Bw Turnbull ameongezea kuwa, Australia “haina dhamana” kuwa itapata manowari yoyote mapya yanayo tumia nishati ya nyuklia kitoka Marekani kwa sababu, inategemea jeshi la wanamaji la Marekani kudumisha manowari yake kwanza.

Upinzani wa mseto unakataa kusema kama uta elekea katika uchaguzi, ukitoa ahadi ya kupunguza ushuru wa mapato. Kabla ya kutangazwa kwa bajeti ya shirikisho wiki ijayo, Msemaji wa Hazina wa Peter Dutton, Angus Taylor, amekuwa akisema kuwa mageuzi ya Jim Chalmers kwa awamu ya tatu ya kupunguzwa kwa ushuru yame feli kupunguza unyemeleaji kwa walipa ushuru na imewaacha wafanyakazi wakielekea kulipa dola 8,900 za ziada kwa ushuru kufikia mwisho wa muongo. Bw Taylor amechapisha utafiti unao onesha mfanyakazi wastan nchini Australia, ali lipa dola $3,500 zaidi kwa ushuru katika mwaka wa fedha wa mwaka jana, kabla serikali ya Albanese ishinde uchaguzi mkuu. Wakati huo huo waziri wa nishati Chris Bowen ame eleza shirika la habari la Channel Seven kuwa, upinzani wa mseto unastahili kuwa wazi kuhusu pendekezo za sera zozote kuhusu kupunguzwa kwa ushuru wa mapato.

Waasi wa M23 wanaoungwa mkono na Rwanda wameituhumu serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwa kujaribu kuhujumu mazungumzo ya amani ya ana kwa ana yaliyopangiwa kufanyika nchini Angola. Msemaji wa M23 Lawrence Kanyuka ameituhumu serikali ya Kongo kwa kutumia ndege za kivita na ndege zisizokuwa na rubani kushambulia kwa mabomu maeneo yaliyo na idadi kubwa ya watu katika siku za hivi karibuni. Kanyuka amesema hatua hii ya serikali ya Kongo inaonyeshakwamba wana nia ya kuhujumu mazungumzo hayo yaliyosubiriwa kwa muda. Shirika la habari la Ufaransa AFP halikuweza kuthibitisha madai hayo ya mashambulizi yaliyotolewa na M23 na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo haikujibu ombi la kutoa tamko kutoka kwa shirika hilo.

Katibu katika Wizara ya Masuala ya Nje Korir Sing’oei Jumapili aliandaa mazungumzo ya simu na mwenzake wa Vietnam kuhusiana na juhudi za kumwokoa Mkenya Margaret Nduta anayekabiliwa na hukumu ya kitanzi nchini humo.Bw Singóei alisema Naibu Waziri wa Masuala ya Kigeni Nguyen Minh Hang alimhakikishia kuwa  ombi la Kenya kuwa Nduta asinyongwe lilikuwa likitathmniwa.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service