Chama cha Labor kime tetea uamuzi wake wakuchelewesha taarifa kuhusu gharama za sera yake, baada ya serikali kutangaza kuwa italipia ahadi za uchaguzi. Bw Albanese amesema si ajabu kwa taarifa hiyo kutolewa karibu ya mwisho wa kampeni, akikumbusha umma jinsi upinzani ulio ongozwa na Abbott mwaka wa 2013, ambao ulisubiri hadi siku tatu kabla ya uchaguzi mkuu.
Kikosi kazi kipya kime undwa jimboni New South Wales, kukabiliana na uhalifu kime waweka nguvuni watu kadhaa wanao husishwa namagenge ya pikipiki. Watu saba wakiwa wanaume sita na mwanamke mmoja, walikamatwa katika eneo la Illawarra, Pwani yakusini na kanda ya kaskazini magharibi ya Sydney. Baadhi ya walio kamatwa ni pamoja na mmoja wa viongozi wa tawi la kusinimagharibi wa genge la Comancheros.
Washirika wa kimataifa wa Somalia Jumatatu wamepongeza kuchaguliwa kwa Hassan Sheikh Mohamud rais ajaye wa taifa hilo. Mohamud anachukua madaraka baada ya miezi kadhaa ya ukosefu wa uthabiti wa kisiasa, huku nchi hiyo ikikabiliwa na uasi wenye ghasia na ukame mbaya. Wakaazi katika mji mkuu, Mogadishu waliingia mitaani wakiimba na kugonga makopo na kufyatua fataki hewani kusherehekea matokeo ya uchaguzi yaliyotangazwa majira ya saa sita usiku.