Taarifa ya Habari 18 Machi 2025

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Shinikizo lakisiasa lina ongezeka kwa chama cha Labor kiache makubaliano ya AUKUS, ambayo kupitia makubaliano hayo Australia inafaa pata manowari ya nyuklia.


Waziri Mkuu wa Zamani Malcolm Turnbull na Kiongozi wa chama cha Greens Adam Bandt, ni miongoni mwa viongozi ambao wame hamasisha serikali ifute mkataba huo na Marekani pamoja na Uingereza, ambao tayari umegharimu milioni $800.

Wiki moja kabla yakutoa bajeti ya shirikisho, Mweka Hazina Jim Chalmers ame gusia hatua kutoka serikali ya Marekani, kama nguvu kubwa inayochochea kujuaji wa uchumi nchini Australia. Bw Chalmers ame elezea ushuru za Marekani wa asilimia 25 kwa vyuma vya Australia kama hasara na, amesema wakati Australia inastahili tarajia mema zaidi kwa washirika wake, matokeo mabaya yata dhibitiwa.

Maelfu ya wanawake nchini Australia wanatarajiwa kufaidi kutoka kwa hatua yakupunguza gharama ya tiba mpya ya endometriosis. Takriban mwanamke mmoja kati ya wanawake saba nchini Australia, hu ugua endometriosis, ambapo tishu zinazo fanana na utando wa tumbo la uzazi, hukua katika sehemu nyingine ya mwili, naku athiri uzazi pamoja nakusababisha maumivu mengi. Serikali imesema tiba mpya ya ugonjwa huo kwa jina la, Ryeqo, ita ongezwa katika mpango wa faida za dawa tarehe 1 Mei na, inatarajiwa kuboresha maisha ya takriban wanawake elfu 8500.

Rwanda imetangaza hivi leo kuvunja uhusiano wa kidiplomasia na Ubelgiji, ikisema taifa hilo la Ulaya "limekuwa likiidhoofisha" nchi hiyo wakati mzozo ukiendelea mashariki mwa Kongo. Wakati huohuo, Ubelgiji nayo imetangaza kuwafurusha wanadiplomasia wa Rwanda huku waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Maxime Prevot akitaja kusikitishwa na uamuzi huo wa Rwanda akisema hauna uwiano na inaonyesha kuwa nchi hiyo haipendelei kushiriki kwenye mazungumzo.

Katibau katika Wizara ya Mashauri ya Kigeni Korir Sing’oei Jumapili aliandaa mazungumzo ya simu na mwenzake wa Vietnam kuhusiana na juhudi za kumwokoa Mkenya Margaret Nduta anayekabiliwa na hukumu ya kitanzi nchini humo. Bw Sing’oei alisema Naibu Waziri wa Masuala ya Kigeni Nguyen Minh Hang alimhakikishia kuwa ombi la Kenya kuwa Nduta asinyongwe lilikuwa likitathminiwa.

Siku chache baada ya chama tawala nchini Uganda, NRM kutangaza kuyakataa matokeo ya uchaguzi mdogo wa ubunge kwenye eneo la Kawempe, rais Yoweri Museveni, sasa ametangaza kuanza kwa uchunguzi kuhusu vurugu zilizojitokeza wakati wa uchaguzi huo.

Katika taarifa yake aliyochapishwa kupitia ukurasa wake wa kijamii wa X, rais Museveni alisisitiza msimamo wa chama chake kuwa hwakubaliani na matokeo yaliyokipa ushindi chama cha upinzani cha NUP, akidai kulikuwa na udanganyifu.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service