Jeshi la Polisi la Victoria lime mkamata mwanaume mwenye miaka 27, anaye shtumiwa kwa kuendesha gari aina ya Toyota Landcruiser, ndani ya soko jana Jumatano 18 Juni. Wame dai gari hilo lilikuwa lime ibiwa na kuendeshwa ndani ya soko la Northland Shopping Centre katika kitongoji cha Preston katika jaribio laku wakwepa polisi.
Serikali ya New South Wales itafanya vikao mjini Griffith hii leo Alhamisi, kama sehemu ya uchunguzi wayo kwa utumwa wa kisasa katika jimbo hilo. Awali uchunguzi huo, uli elezwa kuwa zaidi ya watu elfu 40, wengi wao wakiwa wafanyakazi ambao ni wahamiaji, wame kwama katika utumwa wa kisasa.
Afisa mmoja wa polisi nchini Kenya amekamatwa mara moja baada ya kumpiga risasi raia asiye na silaha Jumanne katika maandamano ya kupinga ukatili wa polisi yaliyofanyika jijini Nairobi. Ni mara chache ambapo hatua ya dharura kama hiyo imechukuliwa dhidi ya maafisa wa usalama nchini, licha ya historia ndefu ya madai ya mauaji ya kiholela dhidi ya raia katika maandamano. Mwanaume aliyepigwa risasi alionekana akiuza barakoa kabla ya kushambuliwa. Jonah Kariuki Wambui babake Boniface Kariuki aliyepigwa risasi jana Jumanne.
Mfuko wa nchi zinazouza mafuta kwa wingi OPEC, kwa ajili ya Maendeleo ya Kimataifa, umeahidi kutoa zaidi ya dola bilioni moja kuisaidia Afrika na nchi zinazoendelea. Msaada huo ni sehemu ya ahadi ya dola bilioni 2 iliyotolewa na nchi za Kiarabu kwa ajili ya kipindi cha miaka mitano ijayo.