Sheria za New South Wales zaku kabiliana na maandamano zina wekwa chini ya shinikizo ndani ya mahakama kuu ya jimbo hilo. Mwanaharakati Josh Lees ame ipeleka serikali ya New South Wales mahakamani, kwa sababu ya sheria hizo kwa niaba ya shirika la Palestine Action Group, akizua hoji mamlaka ya polisi kuwaondoa watu katika maandamano yanayo dhaniwa kufanywa karibu ya sehemu za ibada. Muswada huo uliwasilishwa na serikali ya jimbo mnamo Februari kama sehemu ya sheria mpya zaku kabiliana na chuki na ubaguzi wa rangi, baada ya mashambulizi kadhaa dhidi ya wayahudi kufanywa kote nchini.
Takwimu za hivi punde za ukosefu wa ajira zilizo tolewa na Ofisi ya Takwimu ya Australia, zime onesha kiwango cha ukosefu wa ajira kinasalia kilipokuwa kwa asilimia 4.1 tangu Mei. Kwa ujumla, takriban ajira 2,500 zilipotezwa kutoka uchumi licha ya utabiri kuwa ajira 20,000 zingepatwa baada ya ajira 89,000 kuundwa katika mwezi wa Aprili. Waziri wa Ajira na Mahusiano ya Kazini Amanda Rishworth, amesema data ya ajira ya wakati wote inaonyesha soko la ajira linalo stahimili.
Wawakilishi wa Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wametia saini rasimu ya makubaliano ya amani, hatua inayolenga kumaliza mapigano yanayoendelea mashariki mwa Kongo. Taarifa ya pamoja kutoka nchi hizo mbili pamoja na Marekani ilitangaza makubaliano hayo Jumatano, yakieleza kuwa mkataba kamili unatarajiwa kutiwa saini rasmi Juni 27.
Mji wa Nairobi, Kenya umetikiswa siku ya Jumanne, Juni 17, na makabiliano kati ya waandamanaji, vikosi vya usalama, na makundi ya raia wenye silaha, waliotajwa kuwa "majambazi." Watu kadhaa wamejeruhiwa. Waandamanaji hao walikuwa wamekusanyika kudai haki kwa Albert Ojwang, mwalimu aliyefariki mapema mwezi Juni alipokuwa kizuizini. Mamia ya wanaume waliokuwa wamejihami kwa fimbo na mijeledi mapema asubuhi walifika kwa pikipiki katikati mwa jiji la Nairobi na kuwashambulia waandamanaji. Waandamanaji walijibu, wengine wakichoma moto pikipiki.