Moja ya kampuni kubwa ya nishati nchini Australia, ime waomba wateja wake msamaha, ikisema kukabiliana na kaboni haizuii au kuondoa madhara yanayo sababishwa na kuchoma mafuta. EnergyAustralia ilitoa taarifa Jumatatu 19 Mei 2025, kufuatia kesi iliyo funguliwa na Parents for Climate ambayo ilikuwa imeratibiwa kusikizwa ndani ya mahakama ya shirikisho ya New South Wales wiki jana.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amewaonya wanaharakati ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki kuingia Tanzania na kutoa matamko yanayoweza kuchochea uvunjifu wa amani katika taifa hilo. Akizungumza wakati wa uzinduzi wa sera ya mambo ya nje, toleo la mwaka 2024, Rais Samia Suluhu Hassan ametumia jukwaa hilo kuwaonya wanaharakati ndani ya ukanda wa Afrika Mashariki kuacha kuingia nchini na kutoa matamko yanayoweza kuvuruga amani ya nchi.
Utawala wa Rais William Ruto umetishia kumtia mbaroni aliyekuwa Naibu Rais Rigathi Gachagua kwa kuchochea ghasia, hatua ambayo ikichuliwa itazidisha uhasama kati ya viongozi hao wawili waliofanya kazi pamoja na kutwaa uongozi wa nchi 2022. Wikendi, Naibu Rais Profesa Kithure Kindiki na Waziri wa Usalama wa Ndani Kipchumba Murkomen walimwonya Bw Gachagua, wakisema anapandisha joto la kisiasa kutimiza ajenda yake ya kisiasa kuelekea uchaguzi wa 2027.