Mageuzi hayo yataongeza vifungo gerezani kwa wezi wamagari, watu wanao fanya uhalifu nakujivuna katika mtandao wa jamii wata adhibiwa na, kuhakikisha mahakimu wanazingatia historia za uhalifu wa watoto wahalifu, wanapo fanya maamuzi kuhusu maombi ya dhamana.
Mwendeshaji wa soko la nishati wa Australia, anaonya kuwa kuegemea kwa mfumo wa umeme wa nchi, hauna uhakika kwa muongo ujao bila kuwa na uwekezaji mpya. Katika taarifa mpya ya soko la umeme wa taifa, AEMO imesema uwekezaji wa wakati katika mfumo huo unahitajika wakati Australi inamaliza utegemeaji wayo wakitamaduni wa uzalishaji wa nishati ya makaa ya mawe. Shirika hilo linasema kuwa angalau vituo vitano vya nishati ya makaa yamawe ambavyo ni 13% ya uwezo wa soko, vinatarajiwa kustaafu katika miaka ijayo.
Utafiti mpya umepata kuwa matangazo ya uuzaji wa bidhaa hatari, na zisizofaa kwa vijana katika mtandoa wakijamii yameongezeka sana. Utafiti huo huliofanywa na vyuo vya Queensland na Monash, ulipata kuwa Facebook na Instagram za vijana wenye umri kati ya miaka 16 hadi 25, zimejaa matangazo ya kamari, pombe na vyakula ambavyo sivya afya nzuri. Watafiti wamesema kuna viungo vya moja kwa moja kati ya matangazo na tabia, nakuwa utafiti wao unaonesha kuwa kampuni za mtandao wa jamii zinawalenga kimakusudi vijana.
Baadhi ya wagombea wa upinzani DRC wameelezea wasiwasi wao kuhusu ucheleweshaji na ukiukaji wa taratibu katika shughuli ya uandikishaji wapiga kura, wakisema inafanywa kwa kuupendelea muungano unaotawala. Zaidi ya wapiga kura milioni 50 wa Kongo wanatakiwa kuandikishwa ifikapo Machi 17, lakini Tume ya Uchaguzi, CENI, siku ya Ijumaa ilisema idadi isiyojulikana na vituo vya kuandikishia katika majimbo 10 havikufikia muda wa mwisho uliowekwa, ambao tayari umeongezwa kwa siku 25.
Umoja wa Mataifa nchini Malawi umezindua ombi la haraka la msaada wa kukabiliana na mlipuko ulioweka rekodi ya kipindupindu ambao mpaka sasa umesababisha vifo vya watu 1,450, na kuambukiza 45,000. Wataalamu wa afya nchini humo wanasema kama hatua za haraka hazita chukuliwa kuongeza juhudi za kukabiliana na hali hiyo, idadi ya maambukizi inaweza kuongezeka mara mbili katika miezi michache ijayo. Umoja wa Mataifa unasema mwito huo wa haraka unahitaji kukusanya dola milioni 45.3 ili kutoa msaada wa kuokoa maelfu ya watu wa Malawi walio taabika na kipindupindu.