Hatua za kulinda watoto zaidi katika huduma za malezi ya watoto, zinatarajiwa kuwa miongoni mwa vipaumbele vya kwanza vya serikali ya shirikisho. Mapendekezo ya mageuzi hayo yanajumuisha kuondoa uwekezaji kutoka vituo vinavyo feli, kutimiza viwango vya usalama.
Kituo cha sheria ya haki za binadam, kina omba serikali ya shirikisho ianzishe sheria ya Haki za binadam ya Australia itakayo toa kinga dhidi ya wanacho ona kuwa ni ukandamizaji wa uhuru wa raia. Kituo hicho kimejiunga na mashirika mengine zaidi ya 150 ambayo yame onya baraza la haki za binadam la Umoja wa Mataifa, kuhusu ongezeko la tisho kwa haki za msingi za Australia kabla ya tathmini kubwa ya Umoja wa Mataifa.
Watu kadhaa wamepoteza maisha siku ya jumapili katika mmomonyoko wa ardhi kwenye mgodi wa madini wa Lomera kaskazini mwa Bukavu, ndani ya Jimbo la Kivu kusini, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Kulingana na walioshuhudia, maporomoko ya ardhi yalizika angalau migodi kumi na tano ya uchimbaji madini haswa dhahabu usiku wa kuamkia jumapili.
Mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Kenya Boniface Mwangi, ambaye anatuhumiwa kuwa na dhima katika maandamano dhidi ya serikali mnamo mwezi Juni, ameachiliwa kwa dhamana. Mwangi alikuwa ameshtakiwa kwa madai ya kumiliki mabomu ya kutoa machozi ambayo bado hayajatumika, simu mbili za mkononi, kompyuta na vijitabu kadhaa vya kutunza kumbukumbu.