Idadi yawa Australia ambao wamejisajili kupokea msaada kuondoka katika ukanda wa Mashariki ya Kati ni takriban 2,900 nchini Iran na 1,300 nchini Israel.
Serikali ya Queensland imepanga kuondoa hatua za kutoa afueni kwa gharama ya maisha, itakapo toa bajeti yake hii leo, na inaelnga ukarabati wa muda mrefu wa bajeti kabla yakuwa mwenyeji wa michezo ya Olimpiki ya 2032.
Nchini Rwanda, mpinzani mkuu wa Paul Kagame yuko mikononi mwa idara za usalama tangu siku ya Alhamisi, Juni 19. Victoire Ingabire anatuhumiwa kushiriki katika kesi ya uvunjifu wa amani iliyoanzishwa mwaka wa 2021. Mpinzani huyo alizungumza mahakamani kabla tu ya kukamatwa kwake, akikana kabisa kuhusika na njama hiyo.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.