Taarifa ya Habari 25 Februari 2025

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili

Bango la taarifa ya habari la SBS Kiswahili Source: SBS / SBS Swahili

Waziri Mkuu amesema serikali ya shirikisho inapitia bajeti "mstari kwa mstari" kupata jinsi yakuwekeza ahadi yake ya Medicare.


Upinzani wa mseto nao umesema uta toa uwekezaji sawia na ahadi ya serikali, uhakikisha huduma tisa kati ya kumi kutoka kwa daktari itakuwa bure ndani ya muongo. Mpango huo wa bilioni $8.5 unajumuisha uwekezaji kwa huduma za ziada milioni 18 bila malipo kutoka kwa ma GP kila mwaka, udhamini wa mafunzo ya wauguzi, na kuongeza fursa za mafunzo yama GP.

Jeshi la Polisi la New South Wales limewakamata na kuwafungulia mashtaka watu 550 katika oparesheni jimboni kote iliyodumu siku nne, ikiwalenga wanao fanya makosa ya unyansaji wa nyumbani na kijinsia. Operasheni Amarok IX ilikamilika Jumamosi 22 Februari 2025, baada ya kuwafungulia zaidi ya mashataka 1000 walio kamatwa.

Data mpya ime onesha kuwa wa Australia wana moja ya viwango vya juu vya utambuzi wa saratani ya matiti duniani ila, watalaam wamesema hali hiyo haistahili kuwa sababu ya kuwa na hofu. Utafiti ulio chapishwa katika jarida la Nature Medicine, ulitazama saratani ya matiti duniani na viwango vya vifo katika nchi 185. Utafiti huo ulipata kuwa Australia na New Zealand zimekuwa zikipunguza viwango vya vifo vinavyo sababishwa na saratani kwa asilimia 2.1 kila mwaka.

Viongozi na wajumbe wa Baraza la Haki za binaadamu la Umoja wa Mataifa wamejumuika mjini Geneva, Uswisi siku ya Jumatatu katika mkutano wa 58 wa Baraza hilo. Viongozi hao wamepaza sauti kuhusu kuporomoka kwa viwango vya haki za binaadamu kote ulimwenguni. Wamesema mfumo wa ulinzi wa kimataifa ulioundwa baada ya Vita vya Pili vya dunia haujawahi kukabiliwa na changamoto kubwa kama wakati huu.

Baada ya zaidi ya wiki moja ya mgomo wa kula, mpinzani wa kihistoria nchini Uganda Kizza Besigye ameanza tena kula, kulingana na mkewe. Mgomo wake ulichochewa baada ya mamlaka kukataa kuhamishia kesi yake katika mahakama ya kiraia, licha ya uamuzi wa Mahakama ya Juu mwishoni mwa mwezi wa Januari. Licha ya mabadiliko haya ya mahakama, washirika wake wa karibu hawana matumaini, kama Harold Kaija, katibu mkuu wa People's Front for Freedom, chama kipya kilichoanzishwa na Besigye, mgombea wa urais mara nne nchini Uganda.

Rais wa zamani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila Jumapili alisema uongozi mbaya wa mrithi wake, Rais Felix Tshisekedi umechangia pakubwa kwa kuzidisha mzozo mashariki mwa nchi. Mzozo huo sio tu kutokana na kusonga mbele kwa kundi la waasi la M23 ambalo inasemekana linaungwa mkono na Rwanda au mvutano kati ya Kinshasa na Kigali, Kabila aliandika katika makala ya maoni kwenye gazeti la Afrika Kusini la Sunday Times.

Share
Follow SBS Swahili

Download our apps
SBS Audio
SBS On Demand

Listen to our podcasts
Independent news and stories connecting you to life in Australia and Swahili-speaking Australians.
Ease into the English language and Australian culture. We make learning English convenient, fun and practical.
Get the latest with our exclusive in-language podcasts on your favourite podcast apps.

Watch on SBS
SBS World News

SBS World News

Take a global view with Australia's most comprehensive world news service