Mwanamke mmoja atafikishwa mahakamani hii leo, kujibu shtuma za kudukua hifadhidata ya chuo chake katika jaribio laku okoa hela zaku egesha gari lake.
Watu 12 wameripotiwa kuuawa na wengine zaidi ya 350, wamejeruhiwa kwenye maandamano ya kuadhimisha mwaka mmoja tangu tukio la Juni 25 ambapo vijana 60 waliuawa walipokuwa wakipinga mswada wa Fedha nchini Kenya.
Mkuu wa majeshi ya Uganda Jenreali Muhoozi Kainerugaba ameamsha hasira ya wapiganaji wazalendo ambapo amechapisha katika mtandao wake wa X nia yake ya kuwalenga wapiganaji hao, ambao ni washirika wa FARDC katika maeneo kadhaa ya mashariki.
Rugby Australia inatumia akili bandia kwa umbo la app ya bure kukabiliana na unyanyaji wa mtandaoni, na unyanyasaji wa wachezaji kupitia mtandao wajamii. App hiyo hutambua moja kwa moja nakufuta maoni yenye madhara, yakuudhi na matusi kutoka akaunti ya mtandao wajamii ya mtumiaji, machapisho au kurasa kwa wakati halisi.