Kiongozi mteule wa New South Wales ame ahidi kuongoza kwa niaba ya watu wote wa jimbo lake, baada yakupata ushindi wakihistoria jana usiku. Chama cha Labor cha Chris Minns, kimevunja matumaini ya chama cha mseto kuongoza kwa awamu ya nne na, kuna elekea kuunda serikali ya wengi baada yakushinda viti 47.
Kiongozi wa Victoria Daniel Andrews atakuwa kiongozi wa kwanza wajimbo nchini Australia kutembelea China, tangu mwanzo wa janga la COVID-19. Bw Andrews ataondoka nchini jioni ya Jumamosi kwa ziara ya siku nne, itakayo jumuisha mikutano ya ngazi za juu kuhusu elimu na biashara mjini Beijing, na katika majimbo dada ya Victoria ya Jiangsu na Sichuan.
Rusesabagina aachiwa huru kwa juhudi za Washington na Kigali, kuachiliwa kwa Paul Rusesabagina, kutoka gereza la Rwanda Ijumaa jioni ni matokeo ya mashauriano ya miezi kadhaa kati ya Washington na Kigali. Ambapo pande zote zikiwa na shauku ya kuweka sawa mambo ya kile walichokitaja kama kudhoofisha uhusiano wao.
Serikali ya Sudan Kusini imewasihi wafanyabiashara na wawekezaji kutoka Tanzania kutumia fursa ya kuangalia maeneo mbali mbali na sekta za madini, mafuta au kilimo na kufikiria ni katika sekta gani wanataka kuwekeza katika taifa hilo changa duniani.