Kiongozi wa New South Wales Chris Minns amesema, malipo ya ugumu wakibinafsi ya $180 kwa kila mtu au $900 kwa kila familia, yata anza kutolewa hivi karibuni kwa wakaazi katika jumuiya zilizo athiriwa na mafuriko. Takriban wakaaji elfu 32,000 kutoka jumuiya 14, wana endelea kutengwa, hata wakati maji ya mafuriko yana pungua.
Kupata matibabu nakusimamia ugonjwa wa A-D-H-D, hivi karibuni itakuwa rahisi kama kumwona GP wako. Mabadiliko ya maagizo ya dawa, yata sababisha wa Australia wengi wanao ishi na ungojwa huo sugu, kuto hitaji tena kumwona mtaalam kwa matibabu yanayo endelea ya ugonjwa huo wa upungufu wa tahadhari.
Rais mstaafu wa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo, Joseph Kabila amewataka raia wa nchi hiyo kupambana na kile amekiita "utawala wa udikteta" kwenye taifa hilo lenye utajiri mkubwa wa rasilimali. Kiongozi wa upinzani nchini Uganda Kizza Besigye anaendelea kuzuiliwa, angalau hadi kufikishwa kwake tena mahakamani Mei 29, 2025. Alikamatwa mwezi Novemba mwaka jana wakati alipokuwa akisafiri nchini Kenya na kuonekana tena siku chache baadaye nchini Uganda, ambako anafunguliwa mashitaka kwa "uhaini," uhalifu unaostahili adhabu ya kifo.
Katika mchezo wa Tennis, mshindi mara 22 wa grand slam Rafael Nadal, ame agwa kwa shangwe, katika sherehe yake yaku staafu katika mchuano wa wazi wa Ufaransa. Nadal alimaliza taaluma yake ya mchezo wa tennis, baada yakuwakilisha Uhispania katika kombe la Davis Novemba mwaka jana. Roger Federer, Novak Djokovic na Andy Murray, wali fika uwanjaji kushiriki katika sherehe hiyo iliyo hudhuriwa na maelfu ya mashabiki.