Bw Albanese amesema Australia itabaki kwa mpango wayo wa sasa hivi kuinua matumizi yake ya ulinzi kutoka asilimia 2 hadi asilimia 2.3 ya pato la taifa kufikia mwaka wa 2034.
Mvulana mwenye miaka 15 amefunguliwa mashtaka ya mauaji kwa shutma yakumdunga kisu mwanaume mwenye miaka 58, katika kitongoji cha kaskazini cha Clayfield.po wasili. Kijana huyo amenyimwa dhamana na anatarajiwa kufika mbele ya mahakama ya watoto mjini Brisbane baadae hii leo.
Kiongozi Mkuu wa Iran, Ayatollah Ali Khamenei, amesema kuwa Iran haitasita kujibu mashambulizi yoyote ya Marekani kwa kuvilenga vituo vya kijeshi vya Marekani vilivyoko katika eneo la Mashariki ya Kati.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya Kipchumba Murkomen amesema kwamba kilichojiri Jumatano 25.06.2025 nchini humo hakikuwa maandamano bali ni ugaidi uliofichwa chini ya mwavuli wa upinzani.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.