Chama cha Labor cha NSW kimetangaza mageuzi kwa huduma ya afya ya akili ya shirika la lifeline, nakuongeza mara mbili ufadhiliu wa huduma za mazungumzo. Tangazo hilo limejiri wakati kuna ongezeko kwa idadi yawa Australia wanao endelea kutegemea huduma za afya ya akili, hususan baada ya janga la UVIKO-19.
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Felix Tshisekedi alisema Jumatatu kwamba mzozo na waasi mashariki mwa nchi hiyo unaweza kuvuruga maandalizi ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika Desemba 20.
Mgombea wa Urais wa chama tawala nchini Nigeria, Bola Tinubu anaongoza kwa kura katika majimbo 20 kati ya 36 nchini Nigeria. Matokeo hayo ya awali ni kwa mujibu wa matokeo ya awali yaliokusanywa na shirika la habari la la Uingereza Reuters. Lakini wapinzani wamelisusia zoezi la kuhesabu kura kwa kuonesha mashaka ya vitendo vya udanganyifu.