Serikali ya Wilaya ya Kaskazini imetangaza sheria zakuruhusu dhana mpya dhidi ya dhamana kwa makosa ya kutumia silaha katika uhalifu. Hatua hiyo imejiri wakati mamia yawa andamanaji walipo jumuika nje ya bunge la Wilaya ya Kaskazini Jumamosi, kuomba hatua kali zaidi kwa uhalifu baada ya mwanaume mmoja kudungwa kisu naku uawa hivi karibuni katika sehemu ya kazi.
Makamu Rais wa Marekani Kamala Harris amekutana na Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo siku ya Jumatatu, akiwa amewasili na kitita cha dola milioni 139 ili kusaidia katika masuala ya usalama, uchumi na maendeleo kwa ajili ya nchi hizo mbili, ikiwa ni sehemu ya ziara hiyo ya mataifa matatu ya Afrika. Ziara hiyo katika nchi za Ghana, Tanzania na Zambia itamalizika tarehe 2 Aprili, inafuatia mkutano wa kilele ulioandaliwa na rais Joe Biden mjini Washington mwezi Desemba na kuhudhuriwa na viongozi kutoka Afrika, ambapo Washington inatarajia kusawazisha ushawishi unaoongezeka wa China na Russia barani Afrika.
Maelfu ya watu wameandamana katika mitaa ya mji mkuu wa Kenya Nairobi licha ya tamko la serikali kuwa maandamano hayo ni kinyume cha sheria. Polisi wametumia mabomu ya machozi kuwatawanya wandaamanaji hao. Kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, aliungana na waandamanaji huko magharibi mwa jiji la Nairobi ambapo msafara wake uliwavuta maelfu ya wafuasi.