Serikali ya New South Wales imesema zaidi ya nusu bilioni ya dola zita tumiwa kukabiliana na unyanyasaji wa nyumbani, wakati serikali inaongeza matumizi kwa magereza na mahakama. Takriban nusu ya pesa zime tengwa kwa huduma ya msaada wa wahanga wenye thamani ya dola milioni 227, kuwasaidia waathirika na wahanga huduma ya ushauri na msaada wakifedha.
Kiongozi wa upinzani nchini DRC Martin Fayulu amezungumza. Katika ujumbe uliotumwa kwenye mitandao ya kijamii mnamo Juni 2, 2025, ametoa "wito wa kuwajibika." Ujumbe huo, wenye wa dakika tatu tu, ambao ni jibu kwa ule uliotumwa na rais wa zamani Joseph Kabila takriban siku kumi kabla.
Wanaharakati Boniface Mwangi (Kenya), na Agather Atuhaire kutoka (Uganda) wame elezea waandishi wa habari masaibu waliyo pitia walipokuwa chini ya ulinzi wa jeshi la polisi la Tanzania siku chache zilizo pita. Wawili hao kwa hisia kubwa na wakitokwa machozi, walifunguka kuhusu unyama walio tendewa pamoja na hatua watakazo chukua kutafuta haki.