Kuanzia Julai 1 wa Australia wata weza pata ufikiaji mkubwa zaidi kwa likizo ya wazazi, kima cha chini cha malipo kita ongezeka na mamilioni wata ongezewa malipo yao ya Centrelink.
Wauguzi jimboni Queensland wanatihsia kufanya mgomo baada ya chama cha wauguzi jimboni humo, kutoa hati ya mwisho ya mpango wa malipo kwa serikali ya jimbo hilo.
Nchini Tanzania, kiongozi wa upinzani Tundu Lissu alifikishwa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam siku ya Ijumaa, Juni 27, 2025, kupinga kifungu cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai. Sheria hii, iliyoanzishwa mwaka wa 2018 kutokana na sheria za kupambana na ugaidi, sasa inaruhusu upande wa mashtaka kuomba kutotajwa kabisa kwa mashahidi-pamoja na maelezo yao-bila kuwafahamisha upande wa utetezi au hata jaji.
Bonyeza hapo juu kwa taarifa kamili.