Sussan Ley amesema aina yake ya uongozi uta tofautiana na mtangulizi wake Peter Dutton, ambapo uongozi wake utalenga ksikiza badala yakutoa somo. Kiongozi huyo wa upinzani ali ambia shirika la habari la ABC, Upinzani wa mseto ambao ume badilika , pamoja na kiongozi wa Nationals David Littleproud, wana wakilisha timu imara inayo ungana.
Rais wa zamani wa DRC Joseph Kabila amekutana na viongozi wa dini Alhamis Mjini Goma, Mji Mkuu wa Kivu Kaskazini wa mashariki mwa Kongo na unaokaliwa na waasi wa M23 wanaosaidwa na Rwanda. Ziara yake imekuja wakati huu Rais huyo wa zamani akikabiliwa na kesi ya uhaini kwa madai ya kuunga mkono kundi la M23, bunge la Seneti likiwa limemuondolea kinga yake ya kutoshtakiwa ambapo sasa anaweza kufunguliwa mashtaka.
Viongozi wa Upinzani wamekataa msamaha uliotolewa na Rais William Ruto wakati wa Maombi ya Kitaifa Jumatano. Wakiongozwa na Kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka ambaye alialika wenzake nyumbani kwake Tseikuru, Kaunti ya Kitui, viongozi hao walisema ombi la msamaha la Ruto lilinuiwa kufumba macho Wakenya baada ya kuhisi kwamba atashindwa kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2027. Bw Musyoka alisema ombi hilo lilikuwa kejeli kubwa kwa familia ambazo bado zinaomboleza watoto wao waliouliwa na risasi za polisi wakati wa Maandamano ya Kupinga Mswada wa Fedha 2024.
Ngugi wa Thiong'o, mwandishi maarufu na msomi kutoka Kenya, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 87. Kifo chake kimethibitishwa na mwanawe, Nducu wa Ngugi, ambaye amesema mwandishi huyo amefariki mjini Bedford, Georgia, ambako alikuwa akipokea matibabu ya figo. Ngugi alikuwa mmoja wa watu mashuhuri zaidi barani Afrika waliotumia kalamu kama silaha ya ukombozi wa kiakili na kijamii.